Fahamu watu waliojenga na kuendeleza mfumo huu wa kisasa
Edward Petro Kipenye (2024) ni mtunzi na mwandaaji wa mafunzo ya Udereva. Amehitimu mafunzo ya Ualimu wa Udereva kutoka VETA Mbeya na kutunukiwa Driving Instructor Certificate of Registration kutoka Kitengo cha Usalama Barabarani – Polisi Makao Makuu.
Anatumia mtaala rasmi wa VETA, alama za barabarani za SADC (1997), na miongozo ya udereva katika kutoa elimu bora kwa wanafunzi wa udereva wa magari madogo na makubwa.
Omari Rashidi ni mbunifu na mjenzi mkuu wa mfumo wa E-Driving. Ana uzoefu mkubwa katika kutengeneza mifumo ya kidigitali kwa shule, taasisi, biashara na maduka, akitumia teknolojia za kisasa na salama.
Ametengeneza mifumo ya kimataifa inayosaidia taasisi kujiendesha kwa ufanisi zaidi kwa kutumia nguvu ya data, AI, na muundo bora wa kiutendaji.